
Kura ya maoni iliyofanywa na taasisi ya YouGov kwa ajili ya shirika la habari la DPA imeonyesha asilimia 49 hawatarajii serikali kumaliza muhula wake, huku asilimia 17 wakitabiri kusambaratika kwa muungano huo mapema mwakani.
Baada ya miezi saba na nusu iliyogubikwa na migogoro, ni asilimia 9 tu ya waliohojiwa wanaamini hali itarejea kawaida mwakani, huku asilimia 49 wakitarajia mvutano kuendelea na asilimia 21 wakiamini hali kuwa mbaya zaidi.
CDU/CSU ilishinda kwa asilimia 28.5 na SPD kwa asilimia 16.4 za kura, lakini pande zote mbili zimeanguka vibaya na kukosa wingi wa kura katika tafiti za karibuni, vyama vya CDU/CSU vikiwa na asilimia kati ya 24 na 27 na SPD kikiwa na asilimia kati ya 13 na 14.