Watoto 130 wa shule nchini Nigeria waliotekwa nyara katika uvamizi wa mwezi Novemba wameachiliwa huru, hatua inayohitimisha moja ya matukio makubwa ya utekaji wa wanafunzi nchini humo katika miaka ya karibuni.

Tukio hilo lilitokea katika shule ya bweni ya St Mary’s Catholic, jimbo la Niger, kaskazini mwa Nigeria. Serikali ya Rais Bola Tinubu imethibitisha kuachiwa kwa wanafunzi hao na kusema wanatarajiwa kufika mjini Minna leo Jumatatu kwa ajili ya kuungana na wazazi wao kabla ya maadhimisho ya Krismasi.

Kuachiliwa kwao kunadaiwa kufuatia operesheni maalum ya kijeshi iliyotumia taarifa za kijasusi. Wanafunzi hao ni sehemu ya zaidi ya wanafunzi 300 na wafanyakazi 12 waliotekwa nyara, huku watoto 50 wakifanikiwa kutoroka.

Mhariri | @claud _jm

#UTV108 #AzamTVUpdates #AdhuhuriLive

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *