Changamoto za vikwazo visivyo vya kikodi pamoja na miundombinu duni katika baadhi ya mipaka ya Tanzania zimetajwa kuchangia ongezeko la foleni, hali inayosababisha athari hasi kwa wafanyabiashara na shughuli za biashara za mipakani. Foleni hizo zimekuwa zikiongeza gharama za usafirishaji, kuchelewesha uingizaji na usafirishaji wa bidhaa, pamoja na kupunguza ufanisi wa biashara.
Akizungumza kuhusu hali hiyo, mchambuzi wa masuala ya biashara na uchumi, Ally Mkimo, amesema vikwazo visivyo vya kikodi vikiwamo taratibu ndefu za ukaguzi na uratibu hafifu kati ya taasisi zinazofanya kazi mipakani vinaongeza muda wa kusubiri kwa wafanyabiashara. Msikilize zaidi hapa
✍Halima Abdallah
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates