Mjumbe maalum wa China katika masuala ya Asia, Deng Xijun, ametoa wito hii leo kwa mataifa ya Thailand na Cambodia kukubaliana kusitisha mapigano na kurudi tena katika meza ya mazungumzo ili kutatua migogoro yao ya mipaka kwa amani.

Katika kipindi cha wiki tatu, Thailand na Cambodia zimekuwa zikishambuliana kwenye mpaka wao wa nchi kavu baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoanzishwa kwa mara ya kwanza na Malaysia na Rais wa Marekani Donald Trump kuvunjika.

Mapema leo, Maly Socheata, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Cambodiaamesema hali katika baadhi ya maeneo bado ni tete

Maly Socheata “Hali katika baadhi ya maeneo bado iko chini ya uvamizi wa kijeshi wa Thailand dhidi ya uhuru wa Cambodia lakini vikosi vyetu vinaendelea kupambana na mchokozi huyo kwa kila hali na tunaendelea kufuatilia hali hiyo kwa karibu na kubaki macho sana.”

Hapo jana, jeshi la Thailand lilisema kwamba Cambodia iliwafyatulia maroketi kadhaa, na kufanya jeshi lake kujibu kwa mashambulizi hayo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *