Foleni katika maeneo ya mipakani imekuwa changamoto ya muda mrefu, hasa mwishoni mwa mwaka, ambapo magari ya mizigo hukwama kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukaguzi wa mizigo na ushuru. Hali hii inasababisha athari kubwa kwa wafanyabiashara, ikiwa ni pamoja na ucheleweshaji wa bidhaa na kupanda kwa gharama za usafirishaji.

Mchambuzi wa Uchumi, Eishante Ephrahim, amesema kuwa changamoto hizi zinahitaji ushirikiano wa mamlaka zote husika ili kupunguza foleni na kuhakikisha biashara inasogea kwa ufanisi zaidi.

✍Halima Abdallah
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *