#HABARI: Mkuu wa Kitengo cha Utalii na Diplomasia Jeshi la Polisi mkoani Arusha SP Waziri Tenga, amesema taarifa za uhalifu dhidi ya watalii zimepungua kwa kiwango kikubwa kwa sasa na hivyo kuifanya sekta ya utalii kukua kwa kasi nchini, na kuwavutia watalii kuja nchini kwa wingi kwa ajili ya kufurahia vivutio vilivyopo wakiwa katika hali ya usalama.

SP Waziri pia amesema huduma zinazotolewa na Polisi wa utalii ni za aina yake, ambazo hazipo mahali pengine popote barani Afrika, hivyo kuifanya sekta ya utalii Tanzania kuwa ya kuvutia zaidi, huku mapato kwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Serikali yakiongezeka.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *