‎#HABARI: Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Joseph Mwakabonga, ameongoza zoezi la ukaguzi wa magari katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Moshi, mkoani Kilimanjaro na kuwataka madereva kuendesha kwa uangalifu na kuzingatia sheria za barabarani ili kuepuka ajali zisizokuwa na ulazima na kwamba Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya dereva yeyote atakayekiuka taratibu hizo.

‎Zoezi hilo limehusisha pia utoaji wa elimu kwa madereva na abiria kuhusu umuhimu wa kufuata sheria za usalama barabarani, hususani katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

‎Amewahimiza abiria kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa pale wanapobaini madereva wanaoendesha kwa uzembe au kukiuka kanuni za usalama barabarani.

‎Katika zoezi hilo, madereva na wamiliki wa vyombo vya moto walipatiwa elimu ya namna ya kuomba stika za mtandao kupitia mfumo wa mimis.tpf.go.tz, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuboresha usimamizi wa usafiri barabarani kwa njia za Kidijitali.


‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *