#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, iliyopo mkoani Songwe, Bw. Hamad Mbega, amesema tayari wameanza utekelezaji wa mpango wa bima ya afya kwa wote, kwa kuanza uandikishaji kwa makundi maalumu ikiwemo watu wenye ulemavu, wazee wasiojiweza pamoja na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Dc Mbega, ameyasema hayo wakati akitoa salamu za sikukuu za mwisho wa mwaka kwa wananchi wa wilaya hiyo ambapo ameongeza kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutimiza ahadi hiyo aliyoitoa kipindi cha kampeni za Uchaguzi Mkuu ya kutimiza jambo hilo ndani ya siku mia moja za mwanzo akiwa madarakani.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *