#HABARI: Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI (Mb) Dkt. Jafar Seif, amewataka vijana wanaojishughulisha na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika maeneo ya Lwamgasa, Nyarugusu, Nyakabwe na Ngula mkoani Geita kujiunga katika vikundi ili kurahisisha utatuzi wa changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo kwa Pamoja.

Dkt. Seif ametoa wito huo kufuatia maombi ya baadhi ya wachimbaji hao waliomuomba afikishe hoja zao kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakisisitiza umuhimu wa wachimbaji wazawa wadogo na wa kati kuendelea kupewa leseni zaidi.

Kwa mujibu wa wachimbaji hao, hatua hiyo itaongeza ajira kwa vijana na kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika jamii zinazozunguka maeneo ya migodi.

Akijibu hoja hizo, Dkt. Seif amesema kuwa suala hilo linaendelea kushughulikiwa na Wizara ya Madini chini ya Mheshimiwa Waziri Anthony Mavunde, na akawahakikishia wachimbaji kuwa serikali inalifanyia kazi.

Ameongeza kuwa kujiunga katika vikundi kutarahisisha upatikanaji wa leseni, akitolea mfano wa kikundi cha Umoja wa Vijana Nyarugusu (UVINYA) ambacho kimefanikiwa kupitia mshikamano na umoja wao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *