‎#HABARI: Waziri wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, amewataka watumishi wa Sekta ya Ardhi nchini, kuepuka kujihusisha na migogoro ya Ardhi, huku akisisitiza kuwa Wizara yake haitavumilia mtumishi yeyote atakayebainika kuwa sehemu ya tatizo.

‎Dkt. Akwilapo alitoa kauli hiyo wilayani Masasi mkoani Mtwara, alipowasili kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

‎Ameeleza kuwa sehemu kubwa ya Migogoro ya Ardhi nchini inachangiwa na baadhi ya watumishi wasiokuwa waadilifu kwa kushirikiana na wananchi, jambo linalosababisha migongano ya mara kwa mara.

‎Pamoja na mambo mengine Dkt. Akwilapo amesema lengo si kufukuza watumishi, bali ni kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa uadilifu atakaye bainika hatua za kinidhamu zitachukuliwa pale itakapobidi.


‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *