Maafisa wa usafirishaji, maarufu kama boda boda, wametakiwa kuacha tabia hatarishi zinazoweza kusababisha ajali barabarani, ikiwemo kupandisha abiria zaidi ya mmoja kwenye pikipiki maarufu mshikaki, hali inayowaweka abiria katika hatari ya kuumia iwapo ajali itatokea.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Katavi, Leopard Fungu, wakati akikagua usalama wa mabasi yanayoondoka mkoani Katavi katika stendi kuu ya Mizengo Pinda.

✍Mwanaidi Waziri
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *