Makundi kadhaa ya kiraia nchini Afrika Kusini yametoa wito yakitaka kupewa dhamana haraka iwezekanavyo wanaharakati wawili watetezi wa Palestina waliogoma kula katika jela za Uingereza yakisema kuwa kuendelea kufungwa raia hao kunahatarisha maisha yao.

Baadhi ya wanaharakati hao watetezi wa Palestina walioko katika mgomo wa kula hadi sasa wamepitisha siku 50 bila chakula na upo uwezekano wa kupoteza maisha ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa.

“Tunaitaka serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer kutafakari juu ya matokeo ya kihistoria ya jibu la Thatcherite kwa mgomo wa kutokua chakula ambao ulisababisha vifo vya Bobby Sands na wafungwa wengine tisa wa kisiasa wa chama cha Republican mnamo mwaka1981,”  yameeleza makundi hayo ya kiraia ya Afrika Kusini.

Yamesema, hatua hiyo inasalia kuwa doa la kimaadili katika historia ya Uingereza na sasa inaonekana kuwa chama cha Labour kinafuata mkondo huo huo.

Wafungwa ho watetezi wa Palestina waliogoma kula wanatuhumiwa kwa kuvamia kampuni tanzu ya Uingereza ya huko Bristol yenye mfungamano na kampuni ya ulinzi ya Israel ya Elbit Systems  kambi ya Jeshi la Wanahewa la Royal huko Oxfordshire.

Makundi ya kiraia ya Afrika Kusini yamesema kuwa watano kati ya watetezi hao wa Palestina walioko katikamgomo wa kula katika jela za Uingereza wana umri chini ya miaka 31, huku mdogo akiwa na umri wa miaka 20, na hali zao za kiafya ni mbaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *