Polisi Mkoa wa njombe wamekamata watu 98 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ikiwemo ubakaji mauaji, Wizi na makosa ya usalama barabarani.
Kamanda wa polisi mkoa wa njombe, Kamishna msaidizi wa polisi ACP. Mahmoud Banga amesema matukio hayo yametokea katika vipindi tofauti kuanzia mwezi Oktoba hadi disemba.
Miongoni mwa watuhumiwa hao yupo Petro mfugale 35yrs akidaiwa kutekeleza Mauaji ya Alfred Mfugale baba yake mzazi, tukio lililotokea tarehe 18.11.2025 akidaiwa kumpigwa na kitu kizito alfred na kumsababishia kifo kile kilichodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.
Tukio lingine linamhusisha Gerold severin miaka 40 mkazi wa Ludewa anaetuhumiwa kufanya matukio ya Ubakaji.
Moja kati ya tukio lililomfanya akatiwa nguvuni ni lile linalodaiwa kufanywa Tar. 24.11.2025 katika kijiji cha madunda wilaya ya Ludewa ambapo mtuhumiwa anadaiwa
Kuvizia wanawake vichakani wakisaka kuni na kuwabaka.
Matukio mengine ni yanayohusisha usalama barabarani ambapo zaidi ya watu elfu tano wamekamatwa njombe kwa kukiuka sheria za usalama barabarani.
Mwandishi @dkhan1410
#HabariStartv.