
Michuano ya kandanda kwa mataifa ya Afrika –AFCON 2025 – inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi leo hii nchini Morocco kwa mechi kadhaa. Wawakilishi wa kanda ya Afrika Mashariki na Kati kwenye michuano hiyo wanatupa karata zao za kwanza uwanjani leo Jumanne.
Mechi ya mapema kabisa ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo dhidi ya Benin majira ya saba na nusu kwa majira ya Morocco. Baadaye jioni, Taifa Stars ya Tanzania itamenyana na Nigeria kwa mchezo unaotazamiwa kuwa mgumu kwa Stars ambayo imekuwa na historia isiyoridhisha kwenye michuano hiyo.
Mechi ya usiku wa leo itakuwa kati ya Uganda na Tunisia.
Hapo jana, Mali iliyo kundi A ililazimishwa sare ya1-1kwenye mchezo wake na Zambia. Bafana Bafana ya Afrika Kusini iliondoka na alama tatu kwa kuichapa Angola mabao 2-1. Matokeo sawa na hayo yalipatikana pia na Mafarao wa Misri walioilaza Zimbabwe bao 2-1.