Akijibu maswali ya waandishi habari mjini Washington, Trump amesema serikali yake itachukua umiliki wa meli hizo na kuashiria kwamba zinaweza kutumika kuhifadhi mafuta.

Tangu Disemba 10, Marekani imezikamata meli mbili za mafuta inazozituhumu kukwepa vikwazo vya Washington kwa biashara ya mafuta ya Venezuela.

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amezitaja hatua hizo za Marekani kuwa “vitendo vya kijambazi na uharamia wa kimataifa”.

Miezi ya karibuni, utawala wa Trump umezidisha shinikizo kwa serikali ya Maduro inayomtuhumu kufadhili biashara haramu ya dawa za kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *