Waziri wa Mambo ya nje  wa Ujerumani Johann Wadephul amesema anaamini kwamba Urusi inaweza kuutumia uwezekano wa kusitisha mapigano nchini Ukraine ili kujiandaa kwa mashambulizi dhidi ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

Akizungumza na shirika la habari la Ujerumani la DPA, kiongozi huyo ametoa tahadhari kwa jumuiya ya NATO kujiandaa kwa uwezekano wa kutokea kwa vita hivyo. 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte, amezihimiza nchi washirika wa Ukraine kuendelea kuiunga mkono nchi hiyo, huku akionya kuwa Ulaya itakabiliwa na hatari kubwa za kiusalama ikiwa azma yao itayumba.

Rutte ameongeza kwamba ni lazima mataifa yaliyomo kwenye NATO yaongeza matumizi ya ulinzi na kutekeleza ahadi zilizokubaliwa na jumuiya hiyo katika mkutano wa kilele wa muungano huo huko The Hague mwezi Juni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *