
Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance amedai kuwa, Ulaya Magharibi yenye silaha za nyuklia inaweza kuwa hatari kubwa ya kiusalama kwa Marekani ikiwa utambulisho wa kitaifa wa nchi zake utaendelea kubadilika kutokana na uhamiaji mkubwa unaofanyika katika nchi hizo.
Vance ameuambia mtandao wa habari wa Uingereza wa UnHerd katika mahojiano maalumu, kwamba nchi hiyo na Ufaransa, pamoja na washirika wengine wa Marekani, kwa sasa hawana hisia ya utambulisho wa kitaifa na wanapoteza mafungamano yao ya kiutamaduni na Marekani kutokana na sera zao za uhamiaji.
“Ikiwa wanaruhusu nafsi zao zizidiwe na fikra haribifu sana za kimaadili, utakuwa unaruhusu silaha za nyuklia ziangukie mikononi mwa watu ambao wanaweza kusababisha madhara makubwa sana kwa Marekani,” amedai Vance katika mahojiano hayo.
Makamu huyo wa rais wa Marekani ameendelea kudai kwamba, watu wenye mfungamano na wenye mielekeo ya Kiislamu sasa hivi tayari wanashinda chaguzi za ndani barani Ulaya na akasema “inategemewa kikamilifu” wanasiasa kama hao kupata nguvu kubwa ya kitaifa ndani ya miaka 15 ijayo.
Vance amesema ukosoaji wake wa kile alichokielezea kama “hali ya mgando” barani Ulaya unakusudia kuchochea uchukuaji hatua, akibainisha uhusiano wa Marekani na ustaarabu wa Ulaya…../