Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen na serikali nchini humo inayotambuliwa kimataifa wamekubaliana hii leo kubadilishana wafungwa ambao jumla yao ni karibu watu 3,000. 

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya karibu wiki mbili za mazungumzo kati ya maafisa waYemen kutoka pande zote mbili huko Muscat, Oman, ambayo ndiyo mpatanishi muhimu katika mzozo huo uliodumu kwa zaidi ya muongo mmoja.

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Yemen, Hans Grundberg, katika taarifa yake ameyakaribisha makubaliano hayo kama “hatua chanya na yenye maana ambayo ana matumaini kwamba itapunguza mateso ya wafungwa na familia zao kote nchini Yemen.

Waasi wa Houthi wa Yemen wanadhibiti mji mkuu Sanaa na sehemu kubwa ya kaskazini, huku serikali inayotambuliwa kimataifa ikishikilia sehemu kubwa ya kusini na pande hizo zimekuwa vitani tangu mwaka 2015.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *