Wakati gharama za uendeshaji wa magari zikiendelea kupanda kutokana na bei ya mafuta, kampuni ya magari ya GAC kutoka China imetambulisha rasmi suluhisho mbadala la usafiri wa gharama nafuu.
GAC, ambayo ni kampuni ya kimataifa katika ubunifu na teknolojia ya magari, imeletwa nchini na Haofeng International Trade (Tanzania) Ltd, ikiwa na lengo la kuwapatia Watanzania magari yanayochanganya ubora, ufanisi wa mafuta na teknolojia ya kisasa.
Kampuni hiyo imeleta magari yanayotumia mafuta kwa ufanisi mkubwa, magari ya umeme pekee pamoja na yale yanayotumia mfumo wa mchanganyiko wa mafuta na umeme (hybrid).
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, lita moja ya mafuta yenye thamani ya takriban tsh 2,800 inaweza kuendesha gari kwa umbali wa kilometa 100, wakati gari la kawaida la petroli linaweza kugharimu hadi TSh 22,400 kwa umbali huo huo. Kwa magari ya umeme aina ya GAC AION, gharama ya umeme ni takriban TSh 233 pekee kwa umbali wa km 100.
Akizungumza kuhusu ufanisi wa magari hayo, Alfred, Mkurugenzi Mkuu wa Biashara wa GAC, alisema magari hayo ni rafiki kwa maisha ya kila siku.
Magari ya umeme aina ya AION Y na AION V yanatoa uzoefu wa kuendesha wenye utulivu, nguvu na ufanisi mkubwa wa kiuchumi, yakisafiri umbali wa km 500 hadi 600 kwa chaji moja kwa gharama isiyozidi TSh 35,000.