Watoto waliokosa fursa ya Malezi ya wazazi katika kituo cha kulelea watoto yatima na wenye mahitaji maalum Cha Nuru Orphans mkoani Mbeya, wamewaomba wadau kusaidia upatikanaji wa gari la kubeba watoto wanaosoma nje kituo hicho, pamoja na mahitaji ya shule kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.