
Burkina Faso na Equatorial Guinea zinapepetana kwa sasa Desemba 24 kwa mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2025 katika Uwanja wa Mohammed V huko Casablanca. Mechi imeaanza saa 8:30 mchana saa za Afrika ya Kati). Fuatilia mechi moja kwa moja kwenye RFI.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Timu zote mbili hazijafungana ikiwa zimesalia dakika tu chache kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Timu ya taifa ya mchezo wa soka ya Benin, ilianza kwa ushindi katika mchuano wake wa kwanza wa hatua ya makundi, baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0.
Leopard wakichewa siku ya Jumanne, kwenye uwanja wa Al Medina jijini Rabat, walipata bao la mapema, katika dakika ya 16 kipindi cha kwanza, kupitia winga Theo Bongonda.
Ushindi huu ni muhimu kwa DRC ambao wamejipatia alama tatu muhimu katika kundi la D, sawa na mabingwa zamani Simba wa Teranga, ambao waliishinda Botswana 3-0.
Tanzania, Uganda zaanza vibaya
Wakilishi wa Afrika Mashariki, Uganda Cranes na Taifa Stars, zilipoteza mechi za ufunguzi katika kundi C. Tanzania, ilifungwa na Nigeria mabao 2-1. Super Eagles ilianza kwa kupata bao katika dakika ya 36, na Semi Ajayi.
Hata hivyo, Charles M’Mombwa aliisawazishia Taifa Stars katika dakika 50, kipindi cha pili kabla ya Nigeria kupata bao la pili katika dakika ya 52 kupitia Ademola Lookman.
Uganda nayo ilipata kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Tunisia, ambayo ilipata bao la mapema, katika dakika ya 10. Nyota wa mchezo huo, akiwa ni Elias Achouri, aliyeifungia timu yake mabao mawili katika dakika ya 40 na 64.
Bao la Uganda Cranes la kufuta machozi, lilipatikana katika dakika ya 92, kipindi cha muda wa ziada kupitia mshambuliaji Denis Omedi.
Mechi inayofuata inatarajiwa ni mpambano mgumu kati ya Uganda na Tanzania, nchi jirani tarehe 27 katika uwanja wa Al Medina jijini Rabat.