Gabo Zigamba: Jifunze kwa aliyekutanguliaGabo Zigamba: Jifunze kwa aliyekutangulia

MSANII wa Bongo Movie, Gabo Zigamba, amewataka watu kuacha chuki kwa wale waliowatangulia katika maisha au taaluma zao. Akiandika katika ukurasa wake wa Instagram, Gabo amesema watu ambao waliokuzidi kitaaluma ama uzoefu watumiwe kama sehemu ya kujifunza.

“Usimchukie mtu aliyekutangulia, mfanye mfano kama mchonga barabara, kisha jipange vyema kufanikisha malengo yako. Na kama si lazima, basi usifeli hesabu ya mfano,” aliandika. SOMA: Gabo Zigamba awatunuku tuzo waigizaji ‘Baraluko’

Ujumbe huu umepokelewa kwa hisia chanya na mashabiki wengi, wakisema ni funzo muhimu la maisha, hususan kwa vijana wanaojitahidi katika nyanja mbalimbali za kazi na sanaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *