#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Erick Emmanuel, mkazi wa Nzuguni A, kwa tuhuma za kumuua Evance Mtui, mkazi wa Makulu Oysterbay, jijini Dodoma jioni ya Disemba 16, 2025 kwa kutumia kitu chenye ncha nkali.

Jeshi la Polisi limesema lilifanya msako maalum na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo, huku uchunguzi wa kina ukiendelea. Mara baada ya uchunguzi kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi linaendelea kuwasihi wananchi kutoa ushirikiano na kuepuka vitendo vya uhalifu, huku likiahidi kuendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wahalifu.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *