#HABARI: Jumuiya ya Shia Tanzania imewaomba Watanzania kutumia sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya kama chachu ya kuwajenga vijana katika misingi ya uzalendo na kuipenda nchi bila kuangalia tofauti za itikadi za kidini, ikiwa ni sehemu ya kuhimiza mshikamano wa kitaifa na maadili mema kwa jamii nzima.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania, Sheikh Hemed Jalala, amesema ni wakati muafaka kwa Watanzania kurejesha taswira ya nchi iliyokuwa ikisifika kimataifa kama kisiwa cha amani, umoja na mshikamano.
Sheikh Jalala amesisitiza kuwa Tanzania haina mbadala, akibainisha kuwa Waislamu, Wakristo na waumini wa dini nyingine zote ni Watanzania wenye wajibu wa kuilinda na kuijenga nchi yao, Ameongeza kuwa sikukuu hizi ziwe chachu ya kuenzi na kudumisha umoja na mshikamano wa kidini ambao kwa miaka mingi umeifanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.