#HABARI: Watu 14 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la abiria na Lori, baada ya magari hayo kugongana uso kwa uso leo Disemba 24, 2025, katika eneo la Magubike, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Basi hilo lenye namba za usajili T 577 DXL mali ya kampuni ya Nasir Yutong lilikuwa likitokea Tarime kuelekea Dar es Salaam, wakati Lori aina ya Scania lenye namba T 145 AFA / T 148 AFK mali ya kampuni ya ATT likisafiri kutoka Morogoro kwenda Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, akieleza kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi, Alex Patrick (40), mkazi wa Mlandizi,aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine katika eneo lisiloruhusiwa kupita, na kusababisha kugongana uso kwa uso na lori hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda Mkama, majeruhi wa ajali hiyo ni wanawake 3 na wanaume 11, ambao wote wamepelekwa katika Kituo cha Afya Magubike kwa ajili ya matibabu. Dereva wa basi naye ni miongoni mwa waliojeruhiwa na anaendelea kupatiwa matibabu akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.

Powered by #MCHEZOSUPA


JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *