Indonesia yachangia Dola Bilioni 1 Benki ya Maendeleo BRICSIndonesia yachangia Dola Bilioni 1 Benki ya Maendeleo BRICS

INDONESIA imeweka wazi dhamira yake ya kuimarisha ushirikiano wa kifedha kwa nchi zinazoendelea kwa kutangaza mchango wa dola bilioni 1 kwenye Benki ya Maendeleo ya BRICS (NDB). Hatua hii inakuja miezi michache baada ya Indonesia kujiunga rasmi na BRICS Januari 2025, ikitafuta masoko mbadala wakati sera za ushuru za Marekani zikikandamiza bidhaa zake.

Waziri wa Masuala ya Uchumi, Airlangga Hartarto, amesema mchango huu utasaidia kufadhili miradi ya maendeleo endelevu ndani ya bloc ya BRICS na kuonyesha dhamira ya Indonesia ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea. “Serikali imeridhia kutoa dola bilioni 1 kwa uwekezaji katika Benki ya Maendeleo ya BRICS,” alisema Hartarto.

Benki ya Maendeleo ina mtaji wa dola bilioni 100, huku wanachama wa awali Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini wakidhibiti asilimia 94 ya hisa. Benki hiyo tayari imefadhili miradi yenye thamani ya dola bilioni 39, ikijumuisha usafirishaji, nishati safi na maendeleo endelevu. Nchi nyingine wanachama ni Bangladesh, Misri, UAE na Algeria.

Rais wa NDB, Dilma Rousseff, amepongeza Indonesia kwa mchango wake na mafanikio yake katika sekta ya biofuels. “Indonesia ni kiongozi katika biodiesel na imefikia asilimia 40 ya uzalishaji, jambo linalovutia sana,” alisema Rousseff.

Kujiunga kwa Indonesia kunaleta fursa kwa miradi ya kitaifa ikiwemo miundombinu, nishati mbadala na maendeleo ya kidijitali.Hata hivyo, kupunguza utegemezi wa dola ya Marekani ndani ya BRICS bado ni changamoto kutokana na msimamo tofauti wa wanachama na uwepo mkubwa wa dola katika soko la fedha.

Hatua ya Indonesia kuwekeza fedha hizo  ni ishara ya kuendeleza miundo mbadala ya kifedha kwa nchi zinazoendelea, huku ikisaidia uchumi wa Global South kuimarika. SOMA: Ethiopia Yaingia BRICS

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *