Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limeendelea na operesheni maalum za utoaji elimu kwa madereva na watumiaji wa vyombo vya moto, zikiwa na lengo la kuwajengea uelewa na uwezo wa kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.

Akizungumza wakati wa operesheni hizo mjini Karatu, mkoani Arusha, Kamishna wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama Barabarani, ACP Joseph Mwakabonga, amewahimiza madereva kuzingatia kikamilifu sheria za usalama barabarani ikiwemo kuepuka mwendokasi, kutoa risiti za kielektroniki kwa abiria, kutoendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa, pamoja na kuzingatia uvaaji sahihi wa sare kwa madereva wa usafiri wa umma.

✍Ramadhani Mvungi
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *