Klabu ya JKT Tanzania inayoshiriki Ligi kuu ya NBC leo imeshirikia katika zoezi la upimaji macho kwa wachezaji na viongozi wa bechi la ufundi kwa lengo la kuwaweka wachezaji katika uoni mzuri utakao ongeza ushindani usio na mashaka pindi wawapo uwanjani kusaka alama tatu kwenye kila mchezo
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upimaji macho lilifanyika katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni Jijini Dar es salaam ,Mkuu wa kitengo cha Habari JKT Tanzania Masau Bwire amesema ligi kuu ina mechi za usiku na mchana hivyo swala la afya ya macho ni muhimu kuzingatiwa ili mchezaji aweze kukamilisha majukumu yake kwa ufasaha anapokuwa uwanjani