Kocha Appiah ameahidi kwamba kila mchezaji ataweka juhudi zote ili kupata mafanikio kwenye mashindano hayo yanayofanyika nchini Morocco.

Sudan imekuwa katika hali ya mgogoro kati ya jeshi na kikosi cha wanamgambo wa RSF tangu Aprili 2023, mgogoro ambao umeua takribani watu 150,000 na kuwahamisha karibu milioni 14, na hivyo kuunda mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi duniani.

Hata hivyo, kocha Appiah mzaliwa wa Ghana alifanikiwa na timu hiyo kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, licha ya kulazimika kucheza mechi zote za kufuzu ugenini.

Nahodha wa Sudan, Bakhit Khamis, amesema kwamba ingawa hali nyumbani ni ya maafa, wanafurahi kuwa Morocco kwa ajili ya mashindano hayo.

Sudan inashuka dimbani hii leo kukipiga na Algeria. Huku Burkina Faso ikicheza na Guinea ya Ikweta, kisha baadaye Ivory Coast itapimana na Msumbiji na Cameroon ichuane na Gabon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *