.

Chanzo cha picha, Reuters

Maafisa wa
Marekani wamegundua zaidi ya hati milioni moja zaidi zinazoweza kuhusiana na mhalifu
wa kingono marehemu Jeffrey Epstein ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na
watoto, ambazo wanapanga kuzitoa siku zijazo, maafisa wanasema.

Mwanasheria
wa Marekani wa Wilaya ya Kusini ya New York na FBI wameifahamisha Idara ya
Sheria (DoJ) kuhusu ugunduzi huo na kukabidhi hati hizo kwa wanasheria
kuzipitia.

“Tuna
wanasheria wanaofanya kazi saa 24 kupitia na kufanya mabadiliko yoyote
yanayohitajika kisheria ili kuwalinda waathiriwa, na tutatoa hati hizo haraka
iwezekanavyo,” Idara ya sheria ilisema kwenye mitandao ya kijamii
Jumatano.

Idara
ilisema kwamba kutokana na wingi wa nyenzo, mchakato huo unaweza kuchukua “wiki chache zijazo”.

Taarifa hiyo
haikubainisha jinsi waendesha mashtaka wa FBI na New York walivyopata taarifa
hizo za ziada.

Taarifa hizi
zinajitokeza baada ya idara ya sheria kutoa maelfu ya hati wiki iliyopita –
baadhi zikiwa zimefanyiwa marekebisho sana – zinazohusiana na uchunguzi wao
kuhusu Epstein.

Faili hizo
zilitolewa baada ya Bunge kupitisha Sheria ya Uwazi ya Faili za Epstein –
iliyosainiwa na Rais wa Marekani Donald Trump – ambayo iliamuru shirika hilo
kushirikisha hati zote na umma huku likilinda utambulisho wa waathiriwa.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *