
RIPOTI ya afya ya makipa wawili wa Simba imewashtua mabosi wa klabu hiyo na fasta wameanza msako sokoni kutafuta kipa mpya ili kuja kusimama langoni akishirikiana na Hus-sein Abel ambaye amekuwa akipigishwa benchi na wenzake tangu msimu uliopita.
Simba inasaka kipa mpya baada ya ripoti ya makipa kufikishwa kwa kocha mkuu, Steve Bark-er ikionyesha makipa Moussa Camara na Yakoub Suleiman watakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mzima huku klabu hiyo ikikabiliwa na mechi ngumu za michuano inayoshiriki.
Simba ipo katika Ligi Kuu Bara ambayo kwa misimu minne mfululizo haijatwaa taji kama il-ivyo kwa Kombe la Shirikisho (FA), pia ipo Ligi ya Mabingwa Afrika zitakazorejea mwishoni mwa Januari mwakani ilihali timu hiyo ilipoteza mechi mbili za awali za Kundi D na kubu-ruza mkiani kwa sasa.
Simba inalazimika kuingia sokoni kutokana na Yakoub kuumia goti akiwa katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinachoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 inayoendelea Morocco, huku Camara naye akiwa majeruhi kwa muda mrefu kikosini akicheza mechi za raundi ya kwanza za CAF msimu huu dhidi ya Gaborone Utd ya Botswana Septemba mwaka huu.
RIPOTI PASUA KICHWA
Mtihani mkubwa ambao Simba inayo ni michuano ya kimataifa iliyopo hatua ya makundi na itaanza ngwe ijayo kwa kucheza mechi mbili mfululizo na mabingwa wa zamani wa Afrika, Esperance ya Tunisia iliyopo nafasi ya tatu kundini ikiwa na pointi mbili.
Awali, hawakuwa katika presha kubwa baada ya Camara kuumia, kwani mabosi walijua Yakoub atashika usukani vyema akishirikiana na Abel, lakini kuumia kwa kipa huyo akiwa Morocco kumewatibua zaidi kwani kuna uwezekano mkubwa wa kuwakosa wote wawili kwa zaidi ya mwezi.
Taarifa ambazo Mwanaspoti imepenyezewa ni mwamba Yakoub anatakiwa kukaa sio chini ya mwezi mmoja na siku 10, ambapo kwa hesabu atarejea kikosi Februari mwakani kama il-ivyo kwa Camara.
“Yakoub ameumia jeraha sawa kama Camara (goti), ila yeye atakaa nje kwa muda wa mwezi mmoja na siku 10 sio kama Camara ambaye muda wake ulikuwa ni wiki 10,” kilisema chanzo hicho kutoka ndani ya Simba na kuongeza;
“Kuhusu kuumia kwa Yakoub, Simba inataka kupitia upya ripoti za majeraha ya makipa hao wawili ikiwa ni agizo ya kocha mpya, Steve Barker ili wajue wanachotakiwa kufanya haraka kama kusajili kipa mpya au la.”
Mabosi wa Simba vichwa vimeanza kupasuka ili kujua ni nani wanaenda kumsajili ili aweze kurithi nafasi hiyo na kudaka mechi hizo ngumu zilizoko mbele yao.
Mmoja wa viongozi wa klabu hiyo aliliambia Mwanaspoti; “Bahati mbaya wameumia wote kipa namba moja na kipa namba mbili wakati huu tuna ratiba ngumu na kama wataonekana kuchelewa tunataka kusajili kipa haraka.”
Simba itaanza mechi za kimataifa dhidi ya Esperance ya Tunisia Januari 23 ugenini na ku-rudiana Januari 30 mwakani kabla ya kuja kukutana na Petro Atletico Feb 6 na kumalizana na Stade Mallien huku kukiwa na wasiwasi na kuwakosa makipa hao kwa mechi hizo.