Hasira inaongezeka nchini Malawi kufuati ziara ya wiki mbili ambayo mmoja wa makamu wa rais wa nchi hiyo anatarajia kufanya nchini Uingereza baada ya msimu wa likizo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ziara ya Jane Ansah itakuwa ya kibinafsi, lakini ukubwa wa ujumbe wake na gharama ya jumla ya ziara hiyo vimesababisha ukosoaji mkali. Ofisi yake inapinga habari hizi.

Utata huo ulizuka baada ya kutolewa kwa barua inayodaiwa kuvuja, iliyoandikiwa Ubalozi Mkuu wa Malawi jijini London na kusainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje Chauncy Simwaka, ikiorodhesha watu 15 watakaoandamana na Bi. Ansah.

Akiwa madarakani tangu mwezi Oktoba, serikali ya makamu wa rais imeahidi kusimamia uchumi kwa ufanisi na tayari imetangaza mfululizo wa hatua za kubana matumizi.

Vyombo vya habari vya Malawi vimechapisha maelezo zaidi yanayodaiwa kuhusu ziara hiyo, kulingana na hati zilizovuja, zinazoonyesha gharama ya dola laki kadhaa.

Wakati ofisi ya makamu wa rais ikithibitisha ziara hiyo, imepinga habari zinazosambaa kuhusu kiasi cha matumizi ya umma.

“Nyaraka hizi hazitoki katika taasisi yoyote ya serikali na haziendani na rekodi rasmi au matumizi ya umma yaliyoidhinishwa,” amsema Richard Mveriwa, katibu wa habari wa makamu wa rais, katika taarifa.

“Ofisi ya makamu wa rais bado imejitolea kwa uwazi, uwajibikaji, na matumizi ya rasilimali za umma kwa uwajibikaji, na inalaani vikali usambazaji wa makusudi wa taarifa za uongo zinazolenga kupotosha umma.”

Msemaji hakutaja idadi ya watu watakashiriki katika ziara hiyo, ambayo inaripotiwa kuwajumuisha wahasibu wawili, maafisa wanne wa usalama, wasaidizi watatu wa makamu wa rais, na maafisa wengine.

Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu (HRDC), shirika la haki za binadamu la Malawi, unachukulia ukubwa wa ujumbe huo “kuwa wa kutia wasiwasi sana, hasa kwa kuwa ziara hiyo imeelezewa waziwazi kama ya kibinafsi huku ikionekana kufadhiliwa na pesa za umma.”

Ansah alikuwa mgombea mwenza wa Rais Peter Mutharika, ambaye alimshinda rais aliye maluza muda wake Lazarus Chakwera katika uchaguzi wa mwezi Septemba.

Waliahidi “kurudi kwa uongozi uliothibitishwa” wenye uwezo wa kusimamia uchumi vizuri zaidi kuliko utawala wa Chakwera.

Miongoni mwa kupunguzwa kwa matumizi ya umma kulikotangazwa ni pamoja na kupunguzwa kwa ziara za maafisa waandamizi ndani na nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *