
Mkutano wa saa 48 wa wakuu wa nchi wa Muungano wa Mataifa ya Sahel (ESA) umemalizika Jumanne, Desemba 23, katika mji mkuu wa Mali, Bamako. Katika mkutano huu wa pili, Rais wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traoré, Rais wa wa Niger Jenerali Abdourahamane Tiani na Rais wa Mali Jenerali Assimi Goïta walizindua miradi ya pamoja ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo tatu.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Pamoja na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel
Mkutano uliendelea kwa kasi. Wa mwisho kufika nchini Mali, alikuwa Rais wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traoré , ambaye alijiunga haraka na viongozi wengine wawili wa mungano wa ESA.
Kwa pamoja, walizindua makao makuu ya kituo cha televisheni cha ESA cha baadaye. Baadhi ya wafanyakazi wameajiriwa. Matangazo ya kituo hiki yanapaswa kupatikana hivi karibuni. Kitakapoanza kutangaza, kituo hiki cha televisheni kitarusha hotuma rasmi ya Muungano, ambao sasa unasawazishwa kuhusu masuala ya kimataifa.
Kando ya mkutano huo, Jenerali Assimi Goïta alibainisha upatanisho huu wa maono na misimamo kwa waandishi wa habari, “hasa kuhusu kura zetu ndani ya vyombo vya kikanda na kimataifa,” alielezea, kabla ya kuongeza kwamba “ikiwa baadhi ya nchi zitaomba msaada wetu, hili pia litafanyika ndani ya mfumo wa ESA na kwa hivyo litahitaji mashauriano.”
Wakuu hao watatu wa nchi pia walizindua benki ya uwekezaji na maendeleo ya ESA, ambayo inatarajiwa kufanya kazi mwaka ujao.
Mapambano dhidi ya ugaidi yanabaki kuwa kipaumbele ndani ya eneo la ESA. Rais anayeondoka wa shirikisho hilo, Jenerali Assimi Goïta, kwa mfano alizindua amri ya pamoja ya vikosi vya Muungano kando ya mkutano huo. Mara tu itakapoanza kufanya kazi, jukumu lake litakuwa kutetea watu dhidi ya ukosefu wa usalama na wapiganaji wa kijihadi. Rais mpya kaimu wa shirika hilo ni Rais wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traoré.
Kilele cha sherehe hiyo kilikuwa mkutano na viongozi wa nchi hizo tatu. Huku akikiri kwamba “yote si kamilifu na kwamba maendeleo hayawezi kufanywa kwa kasi inayotakiwa,” Kapteni Ibrahim Traoré hata hivyo alibainisha kwamba Muungano “utabadilika.” “Tutashinda ugaidi, tutajiendeleza, na tutajitangaza,” aliahidi. Alihitimisha: “Nchi au kifo, tutashinda!”