Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema asilimia 70 ya makusanyo ya tozo mpya ya uagizaji magari nje ya nchi ‘HIV Response Levy’ itatumika kununua dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI (VVU) na asilimia 30 zitapelekwa katika Mfuko wa Bima ya Afya kwa wote.
Hayo yameelezwa na Meneja Elimu kwa Mlipa Kodi, Paul Walalaze alipozungumza na Joseph Mpangala.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @moseskwindi