Meli mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 2,000 kila moja zimeanza rasmi kutoa huduma katika Bandari ya Karema, mkoani Katavi, hatua inayotarajiwa kuchochea maendeleo ya biashara katika sekta mbalimbali na kukuza uchumi wa mkoa huo.
Kuanzishwa kwa huduma za meli hizo kunalenga kuboresha usafirishaji wa mizigo kupitia Ziwa Tanganyika, kupunguza gharama za usafiri na kuongeza fursa za kibiashara kwa wafanyabiashara na wazalishaji wa ndani ya mkoa wa Katavi na maeneo jirani.
✍ Mwanaidi Waziri
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates