Meya wa Manispaa ya Kibaha, Nicas Mawazo, amemuomba Waziri wa Maji, Ijumaa Aweso, kutembelea eneo la Viziwaziwa ili kujionea hali halisi ya changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama inayowakabili wakazi wa eneo hilo.
Mawazo amesema kuwa wakazi wa Viziwaziwa wamekuwa wakikumbwa na uhaba wa maji kwa zaidi ya miaka kumi, hali inayosababisha usumbufu mkubwa katika maisha yao ya kila siku.
Ameeleza kuwa licha ya kuwepo kwa miundombinu ya mabomba, wananchi wengi hawapati huduma ya maji, huku wakiendelea kupewa bili jambo linalozua mashaka makubwa kuhusu utendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
✍Mariam Songoro
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates