Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Ali Yerlikaya amesema mabaki ya ndege hiyo ya kukodi aina ya Falcon 50 yamepatikana kwenye wilaya ya Haymana nje kidogo ya Ankara.

Taarifa zinasema ndege hiyo ilipata hitilafu ya umeme dakika 16 baada ya kuruka na rubani aliomba kutua kwa dharura lakini hakufanikiwa.
Waziri Mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibah ametoa salamu zake za rambirambi akisema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Luteni Jenerali Mohammed al-Haddad.

Mkuu huyo wa majeshi ya Libya alikuwa nchini Uturuki kwa mazungumzo na viongozi wa ulinzi wa nchi hiyo na mapema hapo jana alikutana na waziri wa ulinzi wa Uturuki Yasar Guler na mkuu wa majeshi ya nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *