Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Netanyahu imesema, Hamas lazima itekeleze kikamilifu makubaliano ya Oktoba, ikibainisha kuwa makubaliano hayo yanatarajia kundi hilo la wanamgambo kuondolewa madarakani Gaza pamoja na kulipokonya silaha na kuondoa misimamo mikali katika eneo hilo. 

Vurugu zimepungua lakini hazijaisha tangu kusitishwa kwa mapigano kuanza tarehe 10 Oktoba, na pande zote zimekuwa zikishutumiana mara kwa mara kwa kukiuka makubaliano hayo. Wizara ya afya ya Gaza inasema Israel imewaua zaidi ya watu 400 katika eneo hilo tangu usitishaji mapigano uanze.

Mpango wa vipengele 20 uliotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump mwezi Septemba unatoa wito wa usitishaji wa awali wa mapigano ukifuatiwa na hatua kuelekea amani pana.

Pande hizo hazijakubaliana kikamilifu juu ya vipengele vyote. Hamas imesema itakubali kuachana na silaha ikiwa taifa la Palestina litakuwa huru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *