“Nimezaliwa kwenye familia ya Mchungaji (baba yangu). Tangu mdogo nilikuwa na uwezo mkubwa sana. Nilikuwa Nina uwezo wa kujitenga porini kwa muda wa siku Tatu.

“Sikuwahi kutamani kuwa Mchungaji wala kuwa na kanisa kwa sababu Watumishi wote waliowahi kuitwa na Mungu tangu zamani na wana familia. Na watoto wengi wa wachungaji hawapendi maisha ya wazazi wao kwa sababu ya ugumu wa maisha.

“Mimi nilikuwa na- focus kusoma kwa bidii ili nikomboe familia yangu kiuchumi. Mwaka wa pili nikiwa chuo kikuu. Nimesomea masomo ya Mathematics na Statistics nilitokewa na kitu ambacho hakionekani nilipata maelekezo nifanye kazi ya Mungu.

“Nilipewa makatazo ya kutokuajiriwa. Nilifuata maelekezo, mwaka 2018 nilianza rasmi huduma. Nilivyotoka Chuo kikuu sikutafuta ajira. Nilianza huduma katika hali ya udogo. Nilianzia Mabibo, nilikuwa nalala chini kwa miezi Sita”- @prophet.edmoundmystic

#LiveonClouds360
#Clouds26Nyoosha
#LainiYaWana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *