KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, ametoa wito wa kusitisha mapigano kwenye maeneo yenye migogoro duniani wakati wa Sikukuu ya Krismasi.

Akizungumza kutoka katika makazi yake ya mapumziko nje kidogo ya mji wa Roma, Papa Leo amesema kwa watu wote wenye nia njema kuhakikisha Krismasi inakuwa siku ya amani, angalau kwa kuonesha heshima kwa siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. SOMA: Papa Leo XIV mwenyeji Tanzania

Aidha, Baba Mtakatifu ameonesha masikitiko yake kwamba Urusi imekataa kusitisha mapigano nchini Ukraine hata katika kipindi hiki cha Krismasi. Wakristo duniani kote wanatarajiwa kusherehekea Sikukuu ya Krismasi kesho Alhamisi, ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *