KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, anatarajiwa kuongoza Misa yake ya kwanza ya Krismasi katika Basilika ya Mtakatifu Petro, mjini Vatican, usiku wa Krismasi. Inatarajiwa kuwa katika ibada hiyo, Baba Mtakatifu atazungumzia umuhimu wa amani duniani, akipaza sauti dhidi ya vita, machafuko na mateso yanayowakumba binadamu katika maeneo mbalimbali yenye migogoro.

Tayari Papa Leo amewahi kutoa kauli kadhaa akitoa wito wa amani na upatanisho, huku akiendelea kuwaombea na kuwakumbuka waathirika wa vita duniani kote. Pia ameziagiza nchi zenye migogoro ya vita itaka kusitisha mapigano ili kuifanya sikukuu ya Krismasi inakuwa siku ya amani angalau kwa kuonesha heshima kwa siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

SOMA: Papa Leo XIV aitaka Dunia kusitisha mapigano Krismasi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *