ol

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Barcelona na Atletico Madrid wako tayari kumsajili beki wa Bournemouth na Argentina, Marcos Senesi, 28, ambaye ameeleza ataondoka klabuni hapo mwaka 2026. (Teamtalk)

Manchester United inamfuatilia winga wa miaka 19 Yan Diomande, ambaye ameichezea timu ya Ivory Coast na thamani yake ikiwa zaidi ya pauni milioni 80 kutoka RB Leipzig . (Talksport)

Manchester United bado hawajafanya mazungumzo na Atletico Madrid kuhusu kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 25, lakini wanajua timu hiyo ya Uhispania iko tayari kumuuza kwa mkataba wa kudumu wa pauni milioni 35. (Mail)

Liverpool inamfuatilia mshambuliaji wa Brentford, Igor Thiago, 24, wanapoangalia wachezaji wa safu ya ushambuliaji. (CaughtOffside)

Newcastle, Nottingham Forest na Crystal Palace zote zinamfuatilia mlinzi wa Ajax mwenye umri wa miaka 22, Youri Baas. (Teamtalk)

Arsenal wanamtaka beki wa kushoto wa AC Milan na Italia, Davide Bartesaghi , 19, ambaye amevutia klabu hiyo ya Serie A msimu huu. (La Gazzetta dello Sport)

Manchester United imepanga kuahirisha uamuzi wowote kuhusu mustakabali wa Mholanzi Joshua Zirkzee huku kikosi chao kikiwa kimebanwa na majeraha na kuondoka kwa wachezaji kwenda kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anawindwa na West Ham na Roma , miongoni mwa wengine. (ESPN)

Pia unaweza kusoma
k

Chanzo cha picha, FAW

Bayern Munich wanamfuatilia mchezaji wa Cardiff, Dylan Lawlor. Akiwa na umri wa miaka 20 Januari 1, beki huyo wa kati tayari amecheza mechi tatu za timu ya taifa ya Wales. (Talksport)

Chelsea , Arsenal na Newcastle zote zinamtaka kiungo wa kati wa Marseille, Mfaransa Darryl Bakola, 18. (Footmercato)

Everton wanachunguza fursa ya kumtoa kwa mkopo beki wa kushoto Adam Aznou, 19, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco bado hajacheza katika timu ya kwanza. (Teamtalk)

Rennes wanalenga kumchukua kwa mkopo kiungo wa kati wa Manchester City , Claudio Echeverri, mwenye umri wa miaka 19, kutoka Argentina, ingawa watakuwa na ushindani kutoka Villarreal na Girona . (Ouest-France)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *