Chanzo cha picha, Getty Images
Muda wa kusoma: Dakika 2
Barcelona wamepunguza kasi ya kumsajili beki wa Crystal Palace Marc Guehi (25) kutokana na gharama kubwa za kifedha, licha ya mkataba wake kumalizika majira yajayo ya joto. (Mundo Deportivo)
Mshambuliaji wa England Marcus Rashford (28) amesema lengo lake kuu ni kubaki Barcelona, ambako yupo kwa mkopo kutoka Manchester United. (Sport via Mirror)
Crystal Palace wanatarajiwa kushindana na West Ham katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Norway Jorgen Strand Larsen (25) kutoka Wolves mwezi Januari. (Telegraph)
Roma wanamfuatilia beki wa Tottenham Radu Dragusin (23) na wanaweza kujaribu kumsajili kwa mkopo wenye kipengele cha kununua moja kwa moja hapo baadaye. (La Gazzetta dello Sport)
Chanzo cha picha, Semenyo
Baada ya Antoine Semenyo kuonyesha mapenzi ya kutaka kujiunga na Manchester City, Liverpool wameelekeza macho yao kwa winga wa Paris St-Germain na Ufaransa Bradley Barcola (23). (CaughtOffside)
Kipa wa Cameroon Andre Onana (29) amesema anafurahia kipindi bora zaidi cha maisha yake tangu ajiunge kwa mkopo na Trabzonspor kutoka Manchester United. (Goal)
Barcelona wanajaribu kumsajili winga kijana wa England Ajay Tavares, anayefikisha miaka 16 mwishoni mwa Desemba, kutoka Norwich City. (Mundo Deportivo)
Bournemouth na Chelsea wote wanamfuatilia beki wa Lazio raia wa Hispania Mario Gila (25). (Il Messaggero)
Sporting Lisbon wanataka kumsajili winga wa West Ham Luis Guilherme (19) kwa mkopo wenye sharti la lazima la kumnunua. (Maisfutebol)
Kocha Unai Emery anaweza kuwa na dirisha tulivu la usajili wa Januari, huku Aston Villa wakiendelea kuwa na wasiwasi kuhusu kanuni za kifedha za Ligi Kuu ya England. (GiveMeSport)
Cologne wanavutiwa na kumrejesha beki wa Leeds Sebastiaan Bornauw (26) katika Bundesliga. (Bild)