Ubelgiji imetangaza kujiunga katika kesi ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya mauaji ya kimbari yaliyofanywa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Katika ufuatiliaji wa kisheria unaoendelea kuhusu vita vya Gaza, Ubelgiji imejiunga rasmi na kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa tuhuma za mauaji ya kimbari. Mahakama ya ICJ imetangaza katika taarifa kwamba Ubelgiji imejiunga na kesi hiyo kwa kuwasilisha “tamko la kuingilia kati.”

Afrika Kusini ilifungua kesi hiyo mwaka wa 2023 baada ya utawala wa kizayuni kuanzisha vita vya kinyama na mauaji ya kimbari, na kusisitiza kuwa mashambulizi hayo ya kikatili ya kijeshi yamekiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari ya 1948.

Oktoba mwaka jana, Pretoria ilikabidhi wasilisho lenye maelezo ya kina kwa mahakama ya The Hague ikionyesha ushahidi wa mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *