Chanzo cha picha, Reuters
Wanajeshi wa
Ukraine wamejiondoa kutoka mji wa mashariki wa Siversk uliokumbwa na vita, huku
Urusi ikiendelea kusonga mbele taratibu.
Jeshi la
Ukraine lilisema Jumanne kwamba lilichukua hatua hiyo “kuokoa maisha ya
wanajeshi wetu na uwezo wa kupigana wa vitengo”, na kuongeza kwamba vikosi
vya Urusi ” vina faidika pakubwa na nguvu kazi”.
Kutekwa kwa mji
wa Siversk kunaileta Urusi karibu na miji ya mwisho iliyosalia ambayo ni “ngome
ya ukanda” wa Sloviansk na Kramatorsk ambayo bado iko mikononi mwa Ukraine
katika eneo la viwanda la Donetsk.
Mapema siku
hiyo, maafisa walisema watu watatu – akiwemo mtoto mdogo – waliuawa katika
shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani za Urusi usiku kucha na makombora
dhidi ya Ukraine.
Urusi
ilianzisha uvamizi kamili dhidi ya Ukraine mnamo Februari 2022, na kwa sasa inadhibiti
takriban 20% ya eneo la Ukraine.
Katika
taarifa, jeshi la Ukraine lilisema wanajeshi wa Urusi wanaendelea na “vitendo vya mashambulizi” katika eneo la Siversk “licha ya kupata
hasara kubwa”.
Iliongeza
kwamba “vikosi vya ulinzi vya Ukraine vilikuwa vimemchosha adui wakati wa
mapigano ya Siversk”.
Kabla ya
uvamizi wa Urusi, Siversk ilikuwa na watu wapatao 11,000.
Wiki mbili
zilizopita Urusi ilikuwa tayari imeripoti udhibiti wa mji huo – lakini Ukraine
ilikana madai hayo wakati huo.
Siversk
imeangamizwa kama mji katika kipindi cha miezi mingi ya mapigano makali.
Soma zaidi: