Wavuvi wa samaki wilayani Ukerewe mkoani Mwanza wameiambia serikali kuwa suluhisho la kumalizika kwa uvuvi haramu lipo mikononi dwa wavuvi wenyewe na serikali inapaswa kusimamia utekelezaji wa mikakati ya kwavuvi katika kukomesha uvuvi huo.

Akitoa kauli hiyo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, mvuvi Frank Mwijarobi amesema kuwa hatua za kukabilina na vitendo hivyo zinapaswa kuanza kuchukuliwa na wavuvi wenyewe kutokana na ukweli kuwa rasilimali watu na nyenzo za kudhibiti uvuvi usiofuata sheria haziwiani na idadi ya watu wanaojishughulisha na vitendo hivyo.

Imeandaliwa na @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *