Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Tarique Rahman, mgombea wa nafasi ya Waziri Mkuu wa Bangladesh, aewasili Dhaka, mji mkuu wa nchi hiyo, siku ya Alhamisi, Desemba 25, 2025, baada ya miaka 17 ya uhamisho wa kujitakia nchini Uingereza, chama chake, Chama cha  Bangladesh Nationalist Party (BNP), kimetangaza kabla ya uchaguzi wa Februari 2026.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tarique Rahman, mwenye umri wa miaka 60, amewakumbatia wafuasi wake alipowasili uwanja wa ndege wa Dhaka, akiandamana na mkewe na binti yake, kulingana na video iliyorushwa hewani na chama cha  Bangladesh Nationalist Party (BNP), ambacho kwa sasa kinaongozwa na mama yake, Waziri Mkuu wa zamani Khaleda Zia.

Awali Chama cha Bangladesh Nationalist Party (BNP) kilisema kinalenga kuwahamasisha hadi wafuasi milioni tano katika mji mkuu kumkaribisha Rahman, ambaye anaonekana sana kama mgombea mkuu wa chama hicho katika uchaguzi wa bunge nchini humo uliopangwa kufanyika mwezi Februari mwakani.

Kuwasili kwake Alhamisi kutoka London kunakuja huku Chama chake cha BNP kikipata nguvu tena baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wake wa muda mrefu, Sheikh Hasina, wakati wa uasi wa wanafunzi mwaka jana.

Rahman, 60, ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani Khaleda Zia na kwa sasa anahudumu kama kaimu mwenyekiti wa BNP.

Tangu mwaka 1991, madaraka nchini Bangladesh yamekuwa yakibadilika kutoka mikononi kati ya Zia na Hasina, isipokuwa vipindi vifupi vya serikali ya mpito. Kwa kuwa chama cha Awami League cha Hasina kiimezuiwa kushiriki katika uchaguzi wa Februari 12, BNP sasa inaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *