s

Chanzo cha picha, Marcel Heijnen

Muda wa kusoma: Dakika 3

Kutoka ”ulezi wa paka” huko Ottoman hadi kuwa walinzi wa mitaani, uhusiano wa Istanbul na paka wake umekuwa wa karne nyingi.

Huko Istanbul, uwiano wa hali ya juu hudumishwa kila siku katika mitaa yake yenye mizunguko, misikiti, vituo vya metro na mikahawa.

Zaidi ya watu milioni 15 wanashindania nafasi katika jiji hilo kubwa zaidi nchini Uturuki, ambalo lipo kati ya Ulaya na Asia pande zote za Bosphorus sawa na paka mwenye maisha nusu nyumbani kwenye sofa na nusu kwenye meza ya kahawa.

Hiyo ndiyo taswira inayofaa, kwa sababu kuna takriban robo milioni ya paka waliopotea wanaoishi hapa pia.

Paka wamefumwa katika vitambaa na katika historia ya jiji kadhalika katika bidhaa kama vile mazulia yanayouzwa kila kona.

“Paka wa Istanbul, kwa ujumla, si wapendwao sana wala wanyama waliopotea, bali ni mchanganyiko wa mtazamo huo,” anasema Marcel Heijnen, mpiga picha na mwandishi wa City Cats of Istanbul, akiongeza kuwa paka hao hawamilikiwi na watu maalum “bali wanatunzwa na jamii katika vitongoji vyao”.

Anabainisha heshima ya paka katika eneo hilo ambayo hajaishuhudiwa kwingineko.

“Kila manispaa ina idara ya mifugo inayosaidia wanyama wa mitaani katika wilaya yao, ikiwa na huduma ya bure ya kuzuia paka wanaozagaa mitaani,” anaelezea Fatih Dağlı, mwanzilishi mwenza wa Jumba la Makumbusho la Paka Istanbul.

“Kliniki binafsi za wanyama pia hutoa huduma kwa bei nafuu kwa paka wa mitaani, na wakazi mara nyingi huchangia kulipia bili za daktari wa wanyama.”

s

Chanzo cha picha, Marcel Heijnen

Kujitolea huku kuhudumia Paka si jambo jipya. “Kuwapenda paka waliopotea kunaanzia wakati Istanbul ilipokuwa chini ya utawala wa Ottoman,” anasema Heijnen.

“Katika kipindi hiki, wenyeji walihakikisha kwamba wanyama waliopotea wanatunzwa.

Upendo huo kwa wanyama waliopotea uligeuka kuwa taaluma ya muda wote wakati kazi inayoitwa mancacı (“mlezi wa paka”) ilipoanzishwa.

Walezi wa paka au mancacı walipewa jukumu la kuhakikisha paka wa jiji hilo wanalishwa, huku wakazi pia wakiwa na chaguo la kununua chakula kutoka kwa mancacı na kuwalisha paka wenyewe.”

Dağlı anafuatilia uhusiano huo zaidi. “Ilikuwa kawaida sana kwa wafanyabiashara wa baharini kuwaweka paka ndani ya meli ili kujilinda dhidi ya panya,” anasema, akiongeza kwamba kadri meli za biashara za hariri na viungo zilivyowasili katika bandari zenye shughuli nyingi huko Istanbul wakati wa enzi za Warumi na Ottoman, ndivyo Paka wengi walivyowasili.

Leo, wakazi wa Istanbul bado wanaishi nao kwa furaha, ndani na nje, juu ya ardhi na chini, katika jiji hilo la paka. Kiasi kwamba jina la utani, “Catstanbul” linatumiwa sana na wapenzi wa paka duniani kote na watalii wengi hufanya safari hapa kwa sababu ya paka.

s

Chanzo cha picha, Marcel Heijnen

Wakati wa ziara zangu, nilifahamu namna, katika jiji hili kubwa na lenye shughuli nyingi, paka wa mitaani wa Istanbul wanavyojithibitisha kuwa raia wake watulivu zaidi.

Iwe nikiwa na benchi la mbao ninapoketi ili kupumzika baada ya matembezi ya kupanda mlima ili kuona Mnara wa Galata au nikiwa nimelala kwenye ukingo wa bahari ninapofurahia kutazama digrii 360 za jiji hilo kutoka baharini, paka wa Istanbul wamenipa hali ya utulivu inayohitajika sana mahali ambapo wakati mwingine panaweza kuhisi kadhia.

Na nimeona paka wengi wakitulia namna hii huku wengine husimama kwa hiari na kupiga mapaja yao kukaribisha, mwaliko wa kirafiki ambao haujui mpaka au kizuizi cha lugha.

Kila mtu, hata paka wanaoishi mitaani, wanastahili wema kama huo.

Kama Heijnen anavyoweza kushuhudia, paka wa Istanbul anapochagua mapaja yako kwa ajili ya kujilaza, huku harufu ya nyama ya kebab, mahindi ya kuchoma na vyakula vingine ikizunguka-zunguka, Istanbul inakuwa eneo la kuvutia zaidi na kupendeza zaidi.

s

Chanzo cha picha, Jeff Bogle

Miji haitambuliki sana kwa utulivu wake. Imejengwa kwa ajili ya watu, imejaa vitu vikubwa kama vile barabara, majengo na madaraja, na imetengenezwa kwa vifaa vigumu kama vile matofali, zege, kioo na chuma. “Kuwa na spishi nyingine hai inayodai nafasi yao katika mchanganyiko huo ni jambo la kipekee sana. Kushuhudia wenyeji wakiwajali viumbe hawa ni jambo la kipekee zaidi,” anasema Heijnen.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *