Cécile Kohler na Jacques Paris wanasherehekea Krismasi na Mwaka Mpya katika Ubalozi wa Ufaransa mjini Tehran, bila uhakika ni lini hatimaye wataweza kurudi nyumbani. Raia hao wawili wa Ufaransa waliachiliwa kutoka gerezani mapema mwezi Novemba, baada ya zaidi ya miaka mitatu ya kizuizini nchini Iran, lakini sakata la kisheria na kidiplomasia halijaisha.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Ni jaribio jingine tena kwao kutumia likizo mbali na wapendwa wao,” anasema mwakilishi wa familia za Cécile Kohler na Jacques Paris. Raia hao wawili wa Ufaransa waliachiliwa kutoka gerezani mapema mwezi Novemba baada ya zaidi ya miaka mitatu ya kizuizini nchini Iran. Lakini, wakati wakisubiri kutatuliwa kwa matatizo ya kisheria na kidiplomasia yanayozunguka hali yao, wanabaki katika ubalozi wa Ufaransa mjini Tehran. Jamaa zao wanasema wanandoa hao, raia wa Ufaransa wanahisi “wanaungwa mkono vyema” ndani ya jengo la ubalozi wa Ufaransa.

Cécile Kohler na Jacques Paris, ambao walikamatwa mwaka wa 2022 wakati wa ziara ya kitalii, walihukumiwa kifungo cha miaka 20 na 17 jela, mtawalia, hasa kwa ujasusi kwa niaba ya idara za ujasusi za Ufaransa na Israel. Kabla ya kuachiliwa kwao, walitumikia kifungo cha miaka mitatu na nusu jela.

Kurudi kwa raia hao wawili wa Ufaransa kunahusiana na hali ya Mahdieh Esfandiari nchini Ufaransa

Wakati wa ziara yake Paris mwishoni mwa mwaka wa 2025, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi aliweka wazi: kurejea kwa raia hao wawili wa Ufaransa kunahusishwa na mazungumzo ambayo Tehran inadai kuwa imejadiliana na Ufaransa. Kwa hivyo kurejea nyumbani kwa Cécile Kohler na Jacques Paris kutategemea hali ya kisheria ya raia wa Iran, Mahdieh Esfandiari.

Atashtakiwa nchini Ufaransa kuanzia Januari 13 kwa “kuhalalisha kitendo cha ugaidi,” “uchochezi wa moja kwa moja mtandaoni kwa kitendo cha ugaidi,” “matusi ya umma mtandaoni kulingana na asili, kabila, rangi, au dini,” na “kujiunga na wahalifu.” Mamlaka ya Ufaransa inamtuhumu kwa mfululizo wa machapisho mtandaoni kuhusu mashambulizi ya Hamas nchini Israel mnamo Oktoba 7, 2023. Kufikia ripoti za hivi punde, raia huyo wa Iran alikuwa katika makazi ya balozi wa Jamhuri ya Kiislamu huko Paris. Anakabiliwa na hatua ya mahakama ambayo inamzuia kuondoka katika ardhi ya Ufaransa kabla ya kesi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *