
Rais wa Uturuki amesema: “Utawala wa Israel hauheshimu wala kufungamana na ahadi zake na unazuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza kila mara kwa kutumia visingizio mbalimbali.”
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema hayo katika hotuba yake jana Jumatano na kubainisha kwamba, licha ya utekelezaji wa usitishaji mapigano huko Gaza tangu Oktoba 11, matatizo katika maeneo ya makazi ambayo yamegeuzwa kuwa magofu na utawala wa Kizayuni yanaendelea kushuhudiwa.
Erdogan alisisitiza kwamba Israel haitekelezi ahadi zake na inaleta vikwazo na ugumu kila mara katika njia ya misaada ya kibinadamu kuingia Gaza kwa visingizio vya uwongo. Pia aliahidi kwamba msaada wa Ankara kwa Palestina utaongezeka katika miezi ya Rajab, Sha’ban na Ramadhani, na kwamba kamwe Uturuki haitaiacha Gaza kamwe.